1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri yaandaa mkutano kuhusu kumaliza mapigano Gaza

Lilian Mtono
21 Machi 2024

Mawaziri wa serikali kutoka mataifa matano ya Kiarabu wamekutana na maafisa wa Palestina hii leo mjini Cairo kujadiliana mzozo wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4dz29
Uharibifu Ukanda wa Gaza
Uharibifu Ukanda wa Gaza Picha: Ashraf Amra/Anadolu/picture alliance

Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imesema kabla ya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken kwamba mawaziri hao walijadiliana umuhimu wa juhudi za kusimamisha vita vya Gaza na kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano pamoja na kuhakikisha ufikishwaji wa misaada.

Msemaji wa wizara hiyo Ahmed Abuzeid ameandika kwenye mtandao wa X kwamba mkutano huo ulihudhuriwa na mawaziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Saudi Arabia, Qatar na Jordan pamoja na Waziri wa uhusiano wa kimataifa wa Umoja wa Falme za Kiarabu na Mamlaka ya Palestina.

Baadae, maafisa hao walitarajiwa kufanya mazungumzo na Blinken aliyeko Misri katika ziara yake ya sita ya Mashariki ya Kati tangu kuzuka kwa vita kati ya Israel na Hamas mnamo Oktoba 7.