1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiPakistan

CPJ yaitaka Pakistan ichunguze mauaji ya mwandishi wa habari

23 Machi 2024

Shirika la kimataifa la kutetea haki za vyombo vya habari ulimwenguni CPJ limezitaka mamlaka nchini Pakistan kuchunguza mauaji ya hivi karibuni ya mwandishi mmoja wa habari na kuimarisha ulinzi kwa vyombo vya habari.

https://p.dw.com/p/4e3Jx
 Islamabad, Pakistan | Maafisa wa polisi
Maafisa wa jeshi la polisi Pakistan wakiwa kwenye majukumu yaoPicha: Ali Kaifee / DW

Wito wa shirika hilo unatolewa katika wakati huu ambapo kunashuhudiwa mashambulizi dhidi ya waandishi na vyombo vya habari.

Mapema mwezi huu mwandishi wa gazeti la kila siku la Daily Khabrain Jam Saghir Ahmed Lar, aliuwawa kwa kupigwa risasi katika jimbo la Punjab.

Mratibu wa CPJ kanda ya Asia, Beh Lih Yi amesema kwamba serikali ya Pakistan lazima iongeze ulinzi kwa vyombo vya habari na kuhakikisha wanahabari wanafanya kazi yao bila kuhofia kulipiziwa kisasi.

Soma pia:CPJ: Waandishi 99 waliuawa kufuatiamzozo wa Israel-Hamas

Malalamiko ya mashambulizi, vitisho na unyanyasaji mtandaoni dhidi ya waandishi wa habari wanaokosoa jeshi, yamekuwa ya kawaida nchini Pakistan.

Kwa mujibu wa CPJ tangu 1992 waandishi wa habari 64 wameuwawa kwa kuhusishwa na kazi zao nchini Pakistan.