1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cameron aelekea Berlin kujadili mizozo ya Ukraine na Gaza

Amina Mjahid
7 Machi 2024

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Uingereza David Cameron atazungumzia kuimarisha uungaji mkono Ukraine na mikakati ya kufikisha misaada zaidi mjini Gaza, atakapokutana na mwenzake wa Ujerumani, Annalena Baerbock Berlin

https://p.dw.com/p/4dFee
Vikao maalum vya UN kuhusu Ukraine
Cameron na Baerbock watajadili hali ya kiutu Gaza na vita vya Urusi nchini UkrainePicha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Uingereza David Cameron atazungumzia suala la kuimarisha uungaji mkono Ukraine na mikakati ya kufikisha misaada zaidi mjini Gaza, wakati atakapokutana kwa mazungumzo na mwenzake wa Ujerumani, Annalena Baerbock, mjini Berlin.

Mkutano wa viongozi hao wawili unafanyika siku chache baada ya vyombo vya habari vya Urusi, kuchapisha wiki iliyopita mawasiliano ya siri kati ya maafisa wakuu wa jeshi la Ujerumani kuhusu Ukraine, iliyojumuisha taarifa kuhusu operesheni za Uingereza nchini humo.

Katika majadiliano ya kimkakati ya kila mwaka ya Ujerumani na Uingereza, wanadiplomasia hao pia watajadiliana kuhusu msaada wa kijeshi kwa Ukraine na namna ya kuishinikiza Urusi kuachana na uvamizi wake.

Watajadili pia hatua ya kusitishwa mapigano Gaza ilipofikia, msaada kwa watu wa Palestina na namna ya kuzuwia uhamiaji haramu.