1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock na Cameron waisihi Israel ijizuie dhidi ya Iran

18 Aprili 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerubani Annalena Baerbock na mwenzake wa Uingereza David Cameron, wametoa wito wa kujizua baada ya kufanya mazungumzo ya kidiplomasia juu ya mgogoro nchini Israel.

https://p.dw.com/p/4eu0a
Israel | Annalena Baerbock na Benjamin Netanyahu
Waziri wa Mambo ya Nje Ujerumani Annalena Baerbock akiwa na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Picha: Ilia Yefimovich/dpa/picture alliance

Wito huo unatolewa wakati kukiwa na hofu kwamba mvutano wa Iran unaweza kutoka nje ya udhibiti.

Akiwa mjini Tel aviv baada ya kukutana na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na Rais Isaac Herzog, Baerbock aliisihi kwa mara nyingine Israel kuchukua hatua zake kwa busara na uwajibikaji katika kukabiliana na mashambulizi ya Iran.

Kwa upande wake Waziri Cameron amesema anatumai Jerusalem itajibu kwa njia ambayo ni ya busara, vile vile ngumu na ambayo haitazidisha mzozo huo unaovuta nadhari ya kimataifa.

Soma pia:Israel vitani: Baraza la vita lina jukumu gani katika vita hivyo?

Iran ilifanya mashambulizi makubwa ya anga dhidi ya Israel siku ya Jumamosi kwa mamia ya ndege zisizo na rubani na makombora ikujibu shambulio kwenye  ubalozi wake mdogo mjini Damascus.

Jumuiya ya kimataifa imetolea wito kwa pande zote kujizuia ili kuepusha mzozo kuwa mkubwa katika eneo hilo la Mashariki ya kati ambalo bado linatafuta suluhu ya vita kati ya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza.